Psalms 8

Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu.

2 bMidomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeamuru sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.


3 cNikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha,

4 dmwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,
binadamu ni nani hata unamjali?

5 eUmemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,
ukamvika taji ya utukufu na heshima.


6 fUmemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

7 gMifugo na makundi yote pia,
naam, na wanyama wa kondeni,

8 hndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.


9 iEe Bwana, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Copyright information for SwhKC